Serikali haiwezi kuumudu kugharamia vipimo na matibabu ya ugonjwa wa corona kutumia kadi za hazina ya kitaifa ya matibabu NHIF.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa Afya Mutahi Kagwe na afisa mkuu mtendaji wa NHIF Peter Kamunyo ambao wameiambia kamati ya bunge la kitaifa kuhusu afya kuwa ada za vipimo na matibabu ya corona ni ghali mno kwa kampuni za bima kumudu.

Wakifika mbele ya kamati hiyo ya afya chini ya uongozi wa seneta wa Trans Nzoia Michael Mbito, wawili hao wamesema janga la corona halikutarajiwa katika kutengeneza malipo wanayofaa kupata wanaotumia bima ya NHIF n ahata bima zingine.

Wakati uo uo

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kuwafungia watu sio suluhu la kipekee katika kuzuia msambao wa corona.

Badala yake waziri Kagwe amewaambia wabunge kwamba kinachohitajika ni kila mtu kubadilisha tabia na kuzingatia masharti ya usalama kuzuia msambao wa virusi hivyo.

Waziri Kagwe amesema haya alipofika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kujibu maswali kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini.

Na ili kupunguza mamabukizi hayo wizara ya afya inamshauri kila mmoja kuzingata masharti ya usalama ikiwemo kuvalia barakoa kila wakati, kunawa mikono kwa kutumia vieuzi na kuepuka mikusanyiko ya watu anavyoeleza Dkt. Victor Ngani.