Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona imeongezeka na kufika 63,244 baada ya watu wengine 756 kupatikana na ugonjwa huo kati ya sampuli 4,316 zilizopimwa katika muda saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe kupitia taarifa amesema watu wengine 728 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 42,659.

Wagonjwa 19 zaidi wamefariki kutokana na huo katika muda huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,130.

Nairobi inaongoza kwa kuandikisha visa 371, Mombasa 82, Kiambu 52, Busia 39, Uasin Gishu 34, Kajiado 27, Kakamega 18, Nyeri na Machakos 17.

Wagonjwa ambao wangali wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini ni 1,331 huku wengine 5,843 wakishughulikiwa nyumbani.

Wagonjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahututi ni 59, 33 wanasaidiwa na mashine kupumua.