Baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu sasa wanasema wanaipinga ripoti ya BBI na wanawataka wakenya kuiangusha.

Vijana hao wakiongozwa na Makori Orina almaarufu Malema wanasema maoni yao hayakujumuisha kwenye ripoti ya mwisho iliyozinduliwa hivi majuzi na badala yake wanasema wazee ndio wamepewa kipaumbele.

Vijana hao wanasema pendekezo la miaka minne la kutolipa mikopo ya HELB si suluhu kwani wanasema ni kazi kupata kazi Kenya.

Wakati uo huo,

Baadhi ya watu wanaoishi na ulemavu wanasema ripoti ya BBI imekosa kuweka bayana mikakati ya kushughulikia mahitaji yao.

Wakiongozwa na mwenyekiti  wa muungano wao  kaunti ya Busia Ronald Obiero, watu hao wanaoishi na ulemavu wanataka kipengee kuwahusu kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kuwa haki zao zinalindwa ipasavyo.