Gavana wa Pokot Magharibi Profesa John Lonyangapuo sasa anaitaka serikali kutafsiri ripoti ya BBI kwa lugha mbalimbali za mama.

Akizungumza baada ya kikao na viongozi mbalimbali kutoka kaunti hiyo walioapa kuunga mkono ripoti hiyo, Lonyangapuo anasema kutafsiriwa kwa ripoti hiyo kwa lugha za mama kutatoa fursa kwa wakenya wote kusoma na kuielewa ili kufanya uamuzi mwafaka kuihusu.