Wakili Paul Gicheru ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kwa tuhuma za kuhitilafiana na mashahidi amejisalimisha katika mahakama hiyo nchini Uholanzi.

Katika taraifa, mahakama hiyo iliyoko jijini The Hague imedhibitisha kuwa Gicheru amejiwasilisha hii leo na anatazamiwa kufunguliwa mashtaka ya kutumia njia za kifisadi kuhitilafiana na mashahidi kwenye kesi ya vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Mahakama hiyo ilitoa waranti ya kukamatwa kwa Gicheru na Philip Kipkoech Bett mwaka 2015 ili wafunguliwe mashtaka ya kujaribu kuzuia utekelezaji wa haki.

Mwendesha mkuu wa mahakama hiyo Fatou Bensouda anaamini kuwa wawili hao walihitilafiana na mashahidi sita wa mahakama hiyo kwa kuwahongwa kati ya Sh5000,000 na Sh5M.

Kwa mujibu wa ICC, zaidi ya watu 1,000 waliuawa wakati wa ghasia hizo, 350,000 walifukuzwa makwao huku wengine 3,500 wakijeruhiwa.