Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala zake za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa kamishna wa polisi Duncan Wachira.

Katika taarifa, amiri jeshi mkuu amemtaja Wachira kama afisa mjasiri na mchapa kazi ambaye alijitolea kulihudumia taifa.

Rais anasema juhudi zake zilisaidia pakubwa kumaliza makundi ya wahalifu haswa jijini Nairobi na kusema kuwa mchango wake kuleta mabadiliko katika idara ya polisi daima utakumbukwa.

Wachira alihudumu kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 1998.

Haijabainika wazi kilichosabbaisha kifo cha mwendazake ambaye anaripotiwa kukumbwa na mshtuko wa moyo mwaka uliopita.