Washukiwa wawili  wa wizi wa mabavu  wameuwawa katika kaunti ya Nyeri na makachero wa idara ya upelelezi wa jinai (DCI )

 Wawili hao walionaswa na kamera za siri wakitekeleza wizi katika duka moja la Mpesa,

walipigwa risasi walipokuwa wanatoroka baada ya kufumaniwa na polisi.

DCI inasema washukiwa hao wamenaswa mara si moja na kamera hizo wakitekeleza wizi katika maeneo mbalimbali kaunti ya Meru.

Washukiwa wamekuwa wakitumia pikipiki zenye nambari fiche za usajili na bunduki moja na risasi kadhaa ilinaswa kutoka kwao.