SHIRIKA la fedha duniani (IMF) limetangaza kuwa litatoa dola bilioni hamsini kuzisaidia nchi zilizoathirika na virusi vya corona ambavyo vinaendelea kusambaa katika mataifa mbalimbali Ulimwenguni.
Shirika hilo limeonya kuwa mkurupuko wa virusi hivyo tayari umeathiri ukuaji wa uchumi ikilinganishwa na miaka iliyotangulia.
Virusi hivyo ambavyo vilianzia nchini China vimesambaa katika zaidi ya mataifa 70.
Barani Africa, mataifa ambayo yamedhibitisha kuwa na virusi hivyo ni Algeria, Nigeria, Senegal, Misri, Morocco na Tunisia.
IMF inasema inatoa fedha hizo ili kusaidia mataifa maskini nay ale ya kipato cha kati ambayo mifumo ya huduma zao za afya iko chini.