IEBC yamuidhinisha Boga kuwania ubunge Msambweni

0

Muwaniaji wa kiti cha ubunge Msambweni kwa tiketi ya chama cha ODM Omar Boga ameidhinishwa kuwania wadhifa huo na tume ya uchaguzi IEBC.

Naibu kiongozi wa chama hicho aliyepia gavana wa Mombasa Hassan Joho na seneta wa Siaya James Orengo waliandamana na Boga kupokea idhini ya IEBC kushiriki kwenye uchaguzi huo mdogo utakaoandaliwa Disemba 15.

Boga ameidhinishwa siku moja baada ya mwenzake huru Feisal Bader kuidhinishwa na kuanza kampeini za kujipigia debe akiungwa mkono na wendani wa naibu rais William Ruto.

Wawaniaji wengine kwenye uchaguzi huo ni Marere Wamwachai (National Vision Party), Ali Hassan Mwakulonda (Party of economic Democracy) na Sheikh Mahmoud (Wiper).

Kiti hicho kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Suleiman Dori.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here