IEBC kupokea sahihi za BBI kesho

0

Mahakama kuu imekataa kukubali ombi la mpiga kura mmoja anayeishi ngambo kutaka tume ya uchaguzi IEBC kuzuiliwa kupokea sahihi za BBI kuzikagua.

Mlalamishi James Gitau anayeishi Dallas, Marekani alitaka IEBC na asasi nyingine za kikatiba kuzuiwa kupokea sahihi hizo hadi Wakenya wanaoishi ngambo wajumuishwe.

Hata hivyo jaji Jairus Ngaah amedinda kuridhia ombi hilo na badala yake kumtaka mlalamishi kuwasilisha kesi yenye uzito zaidi kuunga mkono hoja zake.

Hayo yakijiri

Sahihi milioni 5.2 za BBI zilizokusanywa wiki iliyopita zitawasilishwa kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Alhamisi.

Mwenyekiti wa shughuli za ukusanyaji saini hizo na mbunge wa Suna mashariki Junet Mohammed amesema baada ya IEBC kumaliza kuzikagua, mswada huo utawasilishwa kwa mabunge ya kaunti kujadiliwa.

Mbunge huyo wa ODM amesisitiza kuwa hakuna mabadiliko yoyote ambayo yatafanyiwa ripoti hiyo kufuatia ripoti kuwa huenda mabadiliko ziaidi yakafanywa kabla ya kura ya maamuzi kuandaliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here