Idadi ya waliopona corona yaongezeka zaidi

0

Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini imeongezeka na kufikia 23, 202 baada ya watu 605 kupatikana na ugonjwa huo.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema watu hao wamepatikana na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 4,547 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Habari njema ni kwamba watu wengine 587 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 9,327.

Wagonjwa 6 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi maafa kuwa 388.

Nairobi imeandikisha visa 373, Kiambu 35, Migori 25, Busia & Narok 20, Kajiado & Laikipia 16, Nakuru 15, Kakamega 12, Uasin Gishu 11, Machakos 10, Mombasa 9, Samburu 8, Turkana 7, Murang’a & Kericho 5, Taita Taveta 3, Nyeri, Makueni, Kisumu, Kilifi & Elgeyo Marakwet 2, Siaya, Meru, Kitui, Isiolo & Bungoma 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here