Idadi ya waliopona corona yafikia 23,429

0

Watu 165 wamepona kutokana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 23,429.

Katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amedhibitisha kufariki kwa watu watatu zaidi kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 637.

Idadi ya maambukizi nchini imeongezeka na kufikia 36,393 baada ya watu wengine 92 kupatikana na virusi vya corona.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 25, Mombasa 20, Nakuru 8, Garrissa 7, Uasin Gishu 6, Kisumu 5, Kiambu na Turkana 4, Kakamega 3, Machakos ,Kajiado na Busia 2, Nyeri, Kilifi na Taita Taveta 1

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here