Idadi ya watu walioambukizwa virsui vya corona nchini imepita elfu thelathini baada ya watu wengine mia mbili ishirini na mmoja kupatikana na virusi hivyo leo baada ya sampuli 3, 746 kuchunguzwa.
Takwimu kutoka kwa wizara ya afya zinaonyesha kuwa idadi ya walioambukizwa virsui hivyo nchini sasa ni 30, 120.
Watu wawili zaidi wamefariki kutokana na virusi hivyo na kufikishaidadi ya maafa yaliyotokana na virusi hivyo nchini kuwa 474.
Watu wengine 686 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 16, 656.
Ulimwenguni, maambukizi hayo yamefikia 21,828,929 huku watu million 14,565,173 wakipona.
Virusi hivyo hadi kufikia sasa vimesababisha maafa ya watu 773,114 katika mataifa mbalimbali duniani.