Idadi kubwa ya wanaume wapata corona, Nairobi ikiendelea kuongoza

0

Wanaume 539 na wanawake 188 ni miongoni mwa watu 727 waliopatikana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ambaye ameelezea wasiwasi wake kuhusu idadi kubwa ya wanaume wanaoendelea kupata ugonjwa huo anasema hii inafikisha 25,138 idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini hadi kufikia sasa.

Watu wengine 674 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 11,118 huku maafa yakiongezeka na kufikia 413 baada ya watu 14 zaidi kufariki.

Wakati uo huo

Kila kaunti kati ya zote 47 imeripoti angalau kisa cha ugonjwa wa corona kufikia sasa.

Na huku akisisitizia umuhimu wa kila kaunti kuwa tayari kukabiliana na msambao wa ugonjwa huo, waziri wa afya Mutahi Kagwe kwa mara nyingine amewakanya watu wa Nairobi dhidi ya kusafiri kuelekea ushago ili kuepuka msambao wa virusi hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here