Huenda shule zikafunguliwa mwaka huu asema Magoha

0

Serikali iko tayari kubadilisha tarehe za kungufua shule wakati wowote kwa kuzingatia hali ya ugonjwa wa COVID19 nchini amesema waziri wa elimu Profesa George Magoha.

Na huku visa vya ugonjwa huo vikiendelea kupungua katika siku za hivi karibuni, waziri Magoha amesema huenda shule zikafunguliwa mapema badala ya kusubiri hadi mwaka ujao 2021 kama ilivyokuwa imeratibiwa awali.

Profesa Magoha amesema haya alipozuru kaunti ya Migori kukagua maandalizi ya taasisi za masomo kabla ya kufunguliwa tena.

Wakati uo huo

Mzazi mmoja mkaazi wa Nairobi ameishtaki serikali kulalamikia kuendelea kufungwa kwa shule kufuatia janga la kimataifa la corona.

Mlalamishi Enock Aura anaitaka mahakama kuamua kuhusu iwapo rais Uhuru Kenyatta alikuwa sahihi kutangaza kufungwa kwa shule wakati wa hotuba yake kwa taifa pasipo kuchapisha katika gazeti rasmi la serikali au kuwasilisha uamuzi huo kwa bunge kujadiliwa mwanzo.

Kuu kwenye ombi lake kwa mahakama ni wizara ya elimu ilazimishwe kufungua taasisi za masomo kuanzia Septemba 1 kwani ndio tarehe ambapo shule zinapaswa kufunguliwa kwa muhula wa masomo.

Mzazi huyo aidha anaitaka mahakama kubaini kuwa kubadilisha baadhi ya shule na kuwa vituo vya karantini ilikiuka kanuni ya afya ya umma.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here