Huenda Kenya ikarejea kwenye ‘lockdown’

0

Upo uwezekano kwamba taifa litalazimika kufunga tena shule na mipaka yake iwapo idadi ya visa vya corona itaendelea kupanda.

Tahadhari hii imetolewa na katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman ambaye anasema msambao wa visa hivyo unaendelea kuongezeka kutokana na mapuuza ya masharti ya usalama.

Dtk. Aman amesema baadhi ya mambo ambayo pakubwa yamechangia kuongezeka kwa visa hivyo ni mikutano ya hadhara inayoandaliwa na wanasiasa.

Katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita, watu 318 wamepatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 41,937.

Dkt. Aman amesema kuwa watu wengine 243 wamepona ugonjwa huo huku idadi ya waliopona ikifika 31,340.

Idadi ya maafa imeongeza na kufika 787 baada ya watu 10 zaidi kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Nairobi inaongoza kwa visa 112, Uasin Gishu 30, Mombasa 29, Nakuru 25, Busia 24, Kisii 21,Kisumu 19, Kakamega na Murang’a 8, Kilifi 6, Laikipia, Kiambu, Embu 5, Homabay 4, Trans Nzoia na Turkana 3, Machakos ,Isiolo, Kajiado 2, Nyandarua, Garissa, Tharaka Nithi, Vihiga na Kirinyaga 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here