HUENDA GHARAMA YA CHETI CHA NDOA IKAPANDA

0

Serikali inalenga kupata mapato kutoka kwa wanandoa wanaolenga kupata vyeti vya kurasimisha  ndoa zao kulingana na agizo la Mwanasheria Mkuu  Dorcas Oduor.

Ofisi ya mwanasheria mkuu imeamuru kuwa vyeti vyote vya ndoa ambazo tayari zimefanyika kuwasilishwa ndani ya siku 30 agizo ambalo limewaacha wachungaji na wasajili wa ndoa katika njia panda.

Agizo hili, pia limeweka makataa ya siku 14 kwa wasajili wa ndoa kuchanganua na kupakia vyeti vyote vya ndoa.

Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa serikalii kuongeza ada za kurasmisha ndoa mara kumi zaidi na ilivyokuwa awali.

Wanandoa ambao walilipa shilingi 5,000 kwa mchakato huo sasa watalipa  shilingi  50,000.

Ongezeko hili kubwa linatazamiwa kuathiri maelfu ya Wakenya, ambao wengi wao tayari wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi nchini.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here