Hotuba ya rais Uhuru Kenyatta yakosolewa

0

Zaidi ya mashirika ishirini ya kijamii yameelezea kutoridhishwa kwao na hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta kwa taifa na haswa ukiukaji wa haki za kibinadamu wakati huu taifa linapambana na janga la covid19.

Viongozi wa mashirika hayo wakiongozwa na Katibu mkuu wa shirika la (CRECO) Joshua Changwony wanasema tangia mwezi wa Novemba, kumekuwa na visa kadhaa vya ukiukaji wa haki za kibinadamu na haswa kutoka kwa polisi wanaohakikisha kuwa masharti ya kuzuia msambao wa virusi hivyo yanatekelezwa.

Changwony anasema agizo la kubuniwa kwa kikosi maalum cha polisi kitakachopewa jukumu la kuhakikisha kuwa wakenya wanafuata masharti hayo huenda pia kikachangia ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Mashirika hayo sasa yanataka maafisa wa polisi kupewa mafunzo kuhusu haki za kibinadamu kabla ya kutumwa kuhakikisha masharti hayo yanafuatwa.

Mashirika hayo yamewatetea baadhi ya wakenya ambao hawavalii barakoa likisema wengine hawawezi kumudu na sasa wanataka serikali za kaunti kusambaza barakoa na sabuni ya kunawa mikono.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here