Rais Uhuru Kenyatta amezindua ujenzi wa hospitali mpya tatu za Level 3 katika mitaa ya Uthiru, Kibra na Mukuru Kwa Reuben jijini Nairobi.
Hospitali hizo zenye uwezo wa kuwa na vitanda kumi na sita na Ishirini na nne zinatazamiwa kujengwa katika maeneo ya Muthua huko Uthiru, Kianda, Kibra na Maendeleo katika mtaa wa Mukuru Kwa Reuben.
Rais Kenyatta amesema hospitali hizo tatu ni miongoni mwa ishirini ambazo zinasimamiwa na (NMS) na zitagharimu shilling million sabini.
Rais alikuwa ameandamana mkurugenzi wa NMS Jenerali Mohamed Badi na viongozi wengine wakuu serikalini.
Rais akiwahutubia mamia ya wenyeji waliojitokeza kumlaki amesema ujenzi wa hospitali hizo ni katika harakati za kubadili sura ya jiji la Nairobi.