HOSPITALI YA NAIROBI YAKATALIA MWILI WA MAREHEMU KUZIKWA

0

Familia moja katika eneo la Ndenderu kaunti ya Kiambu imeamua kufanya ibada ya mazishi ya kumzika mpendwa wao baada ya hospitali moja jijini Nairobi kukatalia mwili huo baada ya kushindwa kulipa Sh18M gharama ya matibabu.

Stephen Njoroge Kimani anasema mwanawe mwenye umri wa miaka 13 alifariki baada ya kuugua saratani ya damu (Leukemia) kwa muda wa miaka miwili kabla ya kifo chake.

Juhudi zao za kutafuta matibabu ya mwanao nchini India na katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta (KNH) zimekosa kuzaa matunda na badala yake ameishia kumpoteza mwanawe mpendwa.

Anasema licha ya kwamba wamejaribu kufanya michango ili kupata pesa za kuwawezesha kukabidhiwa mwili huo, kiasi cha pesa walichopata hakikutosha kwani walifaulu kupata Sh4M pekee juma moja lililopita.

Hata hivyo anasema hospitali ya Gertrude imekataa kata kata kuwapa mwili huo ikisisitiza kuwa ni sharti walipwe gharama yote ya matibabu ndiposa mwili huo uachiliwe.

Wakili Kamau Chege wa mahakama kuu ya Nairobi anasema katiba hairuhusu hospitali yoyote kukataa kuachilia mwili wa marehemu kwani mtu huyo hana umuhimu wowote na kwamba hatua hiyo ni sawa na kuidhulumu kimawazo familia ya mwendazake kwa kuwa kuwa mujibu wa mila na desturi za kiafrika, wanafaa kupewa mwili wao kuuzika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here