HOJA YA KUJADILI MUENENDO WA RAIS RUTO YAWASILISHWA KWENYE SENETI

0
SENETA MAANZO
SENETA DAN MAANZO

Seneta wa kaunti ya Kitui Dan Maanzo amewasilisha hoja ya kujadili mwenendo wa Rais William Ruto.

Kulingana na Maanzo, Ruto ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama ya Kirais kama vile kushughulikia masuala muhimu na changamoto zinazowakabili Wakenya .

Maanzo amesema Rais alikosa kulinda maisha ya Wakenya katika kilele cha maandamano licha ya kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Kitaifa.

”Kuhusu kwamba Kifungu cha 25(a) (c) kinatoa haki na uhuru wa kimsingi ambao HAUWEZI kuwekewa mipaka; haki ya kuachiliwa kutokana na kuteswa na kutendewa kinyama au kudhalilishwa au kuadhibiwa, haki ya kuhukumiwa kwa haki kwa kuzingatia matukio ya hivi majuzi ya kutekwa nyara, kuteswa na kupotea kwa Wakenya,’’ Maanzo alisema katika hoja hiyo.

Mbunge huyo anataka Rais kukanywa kwa kusimamia utekelezaji wa miradi muhimu ya serikali bila kuwashirikisha Wakenya.

”Rais wa Jamhuri ya Kenya na Amiri ametenga sehemu ya Wakenya hali inayozidiha kuzidisha wasiwasi miongoni mwa makundi mbalimbali ya Wakenya kutokana na kutoshirikishwa ipasavyo kwa umma kwenye SHIF, SHA, moduli ya ada ya elimu ya Chuo Kikuu, Mpango wa Makazi nafuu, Ukodishaji wa Viwanja vya Ndege miongoni mwa mambo mengine kinyume na Vifungu 10(2), 119(1), 174(c), 232 (1) ambavyo vinadhalilisha afisi kuu ya Rais wa Jamhuri ya Kenya.”

Haya yanajiri wakati ambapo kuna pendekezo la kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua afisini ambalo linatarajiwa kuwasilishwa Bungeni alasiri ya leo.

Hii pia inaakisi tukio la hivi majuzi ambapo Seneta wa Tana River Danson Mungata aliwasilisha ombi la kumshutumu Gachagua mnamo Septemba 23, 2024 kuhusu tabia yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here