ASASI za uchunguzi nchini zimekanusha tuhuma za kuwepo kwa matafaruku baina yao katika kupambana na ufisadi.
Wakuu wa tume hizo ambazo ni ile ya kupambana na ufisadi EACC, mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma DPP Noordin Hajji na mwenzake wa idara ya upelelezi DCI George Kinoti badala yake wamevilaumu vyombo vya habari kwa kuchochea uhasama baina yao.
Kauli zao zinawadia siku mbili baada ya mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya banadari nchini KPA Daniel Manduku kukamatwa na makachero wa DCI kuhusiana na sakata ya ufisadi na kisha kuachiliwa huru baada ya kufiskishwa mahakamani baada ya DPP na DCI kutofautiana kuhusu mashtaka dhidi yake.