Hatma ya Sonko iko kwa Senate

0

Spika wa bunge la Senate Ken Lusaka amepokea rasmi uamuzi wa bunge la kaunti ya Nairobi wa kumuondoa gavana Mike Mbuvi Sonko.

Uamuzi huo umepokezwa kwa Lusaka na spika wa bunge la Nairobi Benson Mutura.

Lusaka amesema anafanya mashauriano na kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo Samwel Poghisio na mwenzake wa walio wachache James Orengo kupanga tarehe ya kuandaa kikao maalum kuamua hatma ya Sonko kwa muda wa wiki moja.

Wawakilishi wadi 88 walipiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumbandua Sonko licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama.

Hoja hiyo iliyowasilishwa bungeni na kiongozi wa walio wachache Michael Ogada akimtuhumu Sonko kwa matumizi mabaya ya afisi na ufisadi.

Wakati uo huo

Aliyekuwa mbunge wa Dagoreti Kusini Dennis Waweru ameashiria kuwa yuko tayari kumrithi Sonko kama gavana wa Nairobi iwapo rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga watamuunga mkono.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here