Hatma ya shule kufunguliwa kubainika Jumatano, asema Magoha

0

Mwelekeo kuhusu kufunguliwa kwa shule utapatikana baada ya mkutano utakaongozwa na rais Uhuru Kenyatta Jumatano hii kujadili hali ya corona nchini.

Kauli hii imetolewa na waziri wa elimu George Magoha aliyezuru shule ya msingi ya Mukuru jijini Nairobi ambapo ameashiria kuhusu uwezekano wa shule kufunguliwa mapema kinyume na ilivyotarajiwa.

Waziri Magoha ambaye amesema shule zitaendelea kupata madawati anasisitiza kwamba licha ya walimu na wachache kupata corona amesema serikali inashughulikia swala hilo na hivyo wazazi hawana sababu ya kuwa na wasiwasi.

Kwa sasa wanafunzi waliorejea shuleni kuendelea na masomo ni wale wa darasa la nne, darasa la nane na kidato cha nne na wanajiandaa kwa mitihani itakayofanyika mwaka ujao wa 2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here