Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amewataka walimu katika shule za umma sawia na zile za kibinafsi kutowarudisha nyumbani wanafunzi kwa sababu ya karo.
Akizungumza katika shule ya msingi ya Olympic, mtaani Kibra Nairobi alipoongoza ufunguzi wa shule, waziri Magoha amesema masomo katika shule za msingi na sekondari ni ya bila malipo isipokuwa shule za bweni ambapo wazazi wanahitajika kulipa.
Magoha amewataka wanafunzi ambao walipata ujauzito wakiwa nyumbani kutohofia kurejea shuleni na kuhaidi kuwa serikali itawapa usaidizi wa kutosha ikiwmeo kupewa muda wa kuenda kujifungua wakati huo ukifika.
Wanafunzi wa kidato cha nne, darasa la nane na wenzao wa darasa la nne wamerejea shuleni hii leo na Magoha ametoa hakikisho kuwa wameweka mikakati ya kuwalinda wasipatwe na virusi vya corona.
Serikali ilifunga shule mwezi Machi mwaka huu baada ya Kenya kurekodi kisa cha kwanza cha corona.