Hatimaye baada ya kutoelewana mara kumi, maseneta wamepitisha kwa kauli moja mfumo utakaotumika kugawa Sh370b katika serikali za kaunti.
Maseneta wamepiga kura kuunga mkono mfumo utakaohakikisha kuwa kila kaunti inafaidika kupitia mfumo utakaotumika.
Mfumo huo uliafikiwa baada ya mashauriano yaliyoongozwa na kamati maalum ya watu kumi na mbili chini ya uongozi wa maseneta Moses Wetangula wa Bungoma na mwenzake wa Nairobi Johnson Sakaja.
Chini ya mfumo huo uliokubalika, hakuna kaunti itakayopoteza mgao wake huku Nairobi ikiongoza kwa kupata kiasi kikubwa cha mgao huo.
Maseneta wamepitisha mfumo huo kufuatia shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali ikiwemo miunagmo ya wahudumu wa afya kufuatia kufungwa kwa shughuli katika serikali za kaunti.









