Hakuna Polisi aliyelazimishwa kutumia pesa zake kununua sare

0

Idara ya Polisi imekanusha taarifa kwamba maafisa wake wamelazimishwa kununua sare mpya zenye rangi ya bluu.

Mkurugenzi wa mawasiliano katika idara hiyo Charles Wahongo amesema hakuna afisa yeyote aliyefukuzwa kazini wala kuamrishwa kutumia pesa zake kununua sare hizo mpya.

Ameongeza kuwa kufikia sasa kuna sare alfu nane ikiwemo alfu sita za Polisi wa kiume na nyingine alfu mbili na maafisa wa kike zinazosubiri kuchukuliwa na kuwataka wale ambao hawajazichukua kufanya hivyo mara moja.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here