Hajji arejesha faili ya KEMSA kwa EACC

0

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji amerejesha faili ya ya uchunguzi kuhusiana na sakata ya ufujaji wa pesa katika shirika la dawa na ununuzi wa vifaa vya matibabu (KEMSA) kwa tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi (EACC) kwa uchunguzi zaidi.

Kwenye taarifa, Haji amesema kuwa afisi yake imepitia faili hiyo kuhusiana na wanaodaiwa kufaidika na sakata hivyo na kubaini kuwa uchunguzi huo uendelee kwani unahusisha watu wengi.

Katika maelezo yake, Haji amesema amebaini kuwa uchunguzi kuhusiana na maafisa sita wakuu wa KEMSA haukuwa wa kuridhisha na kutaka ufanywe kwa undani.

Hayo yanajiri huku rais Kenyatta akisisitiza kwamba lazima hatua kali zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayepatikana kutumia visivyo fedha za umma na haswa kwenye sakata hiyo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here