Kocha mpya wa Harambee Stars ni Jacob ‘Ghost’ Mulee baada ya kujiuzulu kwa Francis Kimanzi.
Kocha huyo ambaye ndiye mkurugenzi mkuu wa Liberty Sports Academy amerejea kuifunza timu ya taifa baada ya miaka kumi.
Aliifuza timu ya taifa mwisho 2010 na kujiuzulu baada ya michezo ya mashirikisho ya Afrika mashariki na kati almaarufu cecafa.
Mulee ambaye hajawaifunza klabu au timu yoyote kwa miaka hiyo kumi alizinduliwa Jumatano asubuhi na shughuli yake kuu ni kuiongoza timu ya taifa Harambee stars kwenye ubingwa wa africa 2021.
Isisahaulike kwamba Mulee aliiongoza timu ya Harambee stars kwenye ubingwa wa Africa mwaka wa 2004.
Mulee ameifunza Tusker FC huku akishinda nao mataji matatu, Apr ya Rwanda na Yanga ya Tanzania.