Ghana: Rais wa zamani Jerry Rawlings afariki

0

Aliyekuwa rais wa Ghana Jerry John Rawlings amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73.

Familia yake imesema marehemu amefariki dunia katika mji mkuu wa Accra baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Jerry Rawlings aliongoza Ghana kwa mihula miwili baada ya kuchaguliwa kati ya 1993-2001 baada ya kustaafu kama mwanajeshi aliyestaafu.

Rais huyo wa zamani aliingia madarakani baada ya kuongoza mapinduzi ya serikali na kukabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia.

Baada ya kumaliza mihula yake miwili, Rawlings alimuidhinisha makamu wake John Atta Mills kuwania urais mwaka huo wa 2001.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here