GAVANA WA BOMET HILLARY BARCHOK ATIWA MBARONI NA E.A.C.C.

0

Gavana wa Bomet Hillary Barchok ametiwa mbaroni na maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuhusiana na uchunguzi wa ufisadi unaoendelea.

EACC imesema kuwa Gavana huyo anatazamiwa kurekodi taarifa katika afisi zake za South Rift jijini Nakuru.

“Barchok, ambaye ni mshukiwa katika kesi hiyo, atasindikizwa hadi katika Ofisi za EACC eneo la South Rift huko Nakuru kwa mahojiano zaidi na kurekodi taarifa,” Msemaji wa EACC Eric Ngumbi amesema.

Kulingana na ripoti , maafisa wa EACC wamevamia nyumba ya gavana huyo wakitafuta stakabadhi zinazohusiana na madai ya ulaghai na ubadhirifu wa fedha katika kaunti hiyo.

Mwaka jana, baadhi ya wabunge kutoka Bomet walitoa wito wa Gavana Barchok kushtakiwa kwa madai ya ufisadi na matumizi mabaya ya pesa katika kaunti.

Wabunge hao wakiongozwa na Seneta Hillary Sigei walimshtumu Barchok kwa usimamizi mbaya wa sekta ya afya kauli yao ikijiri baada ya kifo cha mtoto wa miaka mitatu Ruth Chepng’eno katika hospitali ya Longisa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here