Gavana Obado bado taabani

0

Gavana wa Migori Zachary Okoth Obado, watoto wake wanne pamoja na washukiwa wengine 11 watalala seli hadi Jumatatu wiki ijayo wakisubiri  mahakama kutoa uamuzi kuhusu ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana.

Obado pamoja na wenzake wakiwemo na wanawe Dan, Susan, Jerry na Adhiambo wameshtakiwa kuhusiana na madai ya wizi wa Sh73M ila wamekanusha mashtaka yote 28 dhidi yao.

Hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Lawrence Mugambi alikataa kuridhia ombi la wakili wa washukiwa Kioko Kilukumi kuwaachilia kwa dhamana na badala yake kusukuma uamuzi huo hadi Jumatatu.

Washukiwa wameshtakiwa kwa mashtaka manne ikiwemo kushirikiana kutekeleza ufisadi, ulanguzi wa pesa pamoja na unyakuzi wa mali ya umma

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji anasema watoto wa gavana huyo walitumia Sh38M kulipia karo ya shule na matumizi mengine ya kibinafsi wakiwa nchini Australia, Scotland na Uingereza kando na kunua gari aina ya Toyota V8.

Sh34M pia zinadaiwa kutumika katika ununuzi wa nyumba ya kifahari mtaani Loresho Ridge, Nairobi mmiliki wake akiwa ni bintiye gavana Obado, Evelyn Adhiambo Zachary.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here