Mchakato wa kumuondoa gavana wa Migori Zachary Okoth Obado unatazamiwa kuanza wakati wowote baada ya chama chake cha ODM kuidhinisha kuwasilishwa bungeni kwa hoja ya kutimuliwe kwake.
Chama hicho cha Chungwa kimeafikia uamuzi huu baada ya kukutana na wawakilishi wadi wa kaunti hiyo kwa kuzingatia hatua ya mahakama kumzuia gavana huyo kuingia afisini baada yake kushtakiwa kwa tuhuma za ufisadi.
Gavana Obado vile vile anadaiwa kumtenga naibu wake Nelson Mahanga kwa kumpokonya majukumu na pia kumnyanganya magari rasmi ya serikali hali ambayo imemfanya kukosa kuingia afisini kwa muda wa miezi kadhaa iliyopita.
Obado, watoto wake wanne pamoja na baadhi ya maafisa kaunti waliachiliwa kwa dhamana ya hadi Sh45M baada ya kushtakiwa kwa wizi wa Sh73M.









