Kamati ya bunge la Seneti kuhusu uhasibu imemtaka Inspekta wa Polisi Hillary Mutyambai kumshika gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria kwa kuidharau.
Karani wa bunge Jeremiah Nyengenye katika barua anamtaka Mutyambai kumkamata wa Iria kwa kufeli kufika mbele yake mara kadhaa kujibu maswali kuhusu matumizi ya pesa ya hadi Sh24b mwaka 2014/15 kwenye kaunti yake.
Wiki iliyopita, kamati hiyo ilimtoza faini ya Sh500, 000 gavana huyo baada yake kukosa kufika mbele yake mara tatu.
Kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Kisii Sam Ongeri inaamini kwamba wa Iria anajaribu kuhujumu utendakazi wake kwa kudharau wito wa kufika mbele yake.