GAVANA MWANGAZA AONA GIZA MAHAKAMA IKIDUMISHA KUONDOLEWA KWAKE AFISINI.

0

Gavana wa Meru Kawira Mwangaza amepata pigo baada ya mahakama Kuu kushikilia uhalali wa mchakato wa bunge la seneti wa kumtimua afisini.

Katika uamuzi wake Jaji Bahati Mwamuye amefutilia mbali madai kwamba seneti haikufuata taratibu inayofaa wakati wa kusikiliza na kuamua hoja dhidi YA Mwangaza.

“Mlalamishi ameelezea mifano kadhaa ya kutetea madai kwamba seneti haikusikiza kesi dhidi yake kwa misingi ya sheria. Mahakama haijashawishiwa na maelezo hayo.” Amesema Jaji Mwamuye.

Jaji Mwamuye aidha ameamua kwamba Gavana Mwangaza alikosa kuishawishi mahakama kwamba Bunge la seneti lilimnyima nafasi ya kusikilizwa na kumbagua kwa misingi ya kijinsia.

Jaji huyo amesema kuwa licha ya swala la jinsia kuwa nyeti, ni jukumu la mlalamishi kudhibitisha bila shauku kwamba alibaguliwa.

“Iwapo mlalamishi angedhibitisha hili mahakama hii haingesita hata sekunde moja kutupilia nje mchakato wa kumuondoa afisini.” Jaji Mwamuye ameeleza.

Uamuzi huo unamaanisha kwamba naibu gavana wa Meru Isaac Mutuma M’Ethingia atahudumu kwenye nafasi hiyo iwapo Mwangaza atakosa kukata Rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Mwangaza amekua na mvutano na wawakilishi wadi wa kaunti yake akiondolewa afisini Mara tatu.

Bunge la seneti lilimuokoa mara mbili kabla ya kuafikia uamuzi wa kumtuma nyumbani mwaka jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here