Gavana Muthomi Njuki kushtakiwa, mwenzake Ali Korane akihojiwa kwa ufisadi

0

Gavana wa Tharaka Nithi Onesmus Muthomi Njuki anatazamiwa kushtakiwa baada yake kuhojiwa na makachero wa tume ya maadili na kupambana na ufsadi nchini EACC katika sakata ya shilingi million 34.9.

Gavana Muthomi alijisalimisha katika makao makuu ya EACC baada ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji kuidhinisha afunguliwe mashtaka ya wizi wa mali ya umma.

Njuki anatazamiwa kufunguliwa mashtaka ya ukiukaji wa sheria za utoaji tenda na kusababaisha kupotea kwa pesa za mlipa ushuru.

Yakijiri hayo

Gavana wa Garissa Ali Korane  anatazamiwa kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za ufujaji wa Sh233M pesa za wafadhili.

Pesa hizo zinatajwa kuwa msaada kutoka kwa benki ya dunia zilizofaa kutumika katika kufanikisha miradi ya maendeleo katika kaunti yake.

Inaarifiwa kwamba badala ya kutumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo, pesa hizo zilielekezwa katika akaunti za kibinafsi za gavana huyo na baadhi ya maafisa wa kaunti hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here