Gavana Muthomi Njuki kukamatwa kwa tuhuma za ufisadi

0

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji ameidhinisha kushtakiwa kwa Gavana wa Tharaka Nithi Onesmus Muthomi Njuki kuhusiana na sakata ya shilingi million 34.9.

Katika taarifa, Haji anasema serikali ya Gavana Njuki ilikiuka sheria za utoaji zabuni wakati ilitoa tenda kwa kampuni ya Westomaxx Investment ambayo inahusihwa na Gavana huyo.

Haji ameagiza Gavana huyo na washukiwa wengine kumi na sita ikiwemo maafisa wakuu wa kaunti hiyo kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ufujaji wa pesa za umma.

Haji anasema kampuni hiyo ilitoa stakabadhi ghushi huku kampuni zingine sita zilizotumwa maombi ya kupewa zabuni hiyo zikipuuzwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here