Gavana wa kaunti ya Tharaka Nithi Muthomi Njuki ameachiliwa kwa dhamana ya Sh6M pesa taslimu huku akizuiliwa kuingia afisini mwake.
Hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Milimani Douglas Ogoti amemuachilia gavana huyo pamoja na washtakiwa wenza kwa dhamana baada yao kukanusha kuhusika na sakata ya ufujaji wa Sh34.9M.
Akitoa uamuzi huo, hakimu Ogoti ameshangaa ni vipi visa vya ufisadi vinaendelea kuongezeka kila kuchao wakati ambapo kuna sheria kuhusu namna ambavyo pesa zinafaa kushughulikiwa.
Muthomi amekuwa gavana wa hivi punde kuzuiliwa kuingia afisini mwake baada ya mwenzake wa Migori Okoth Obado aliyeshtakiwa kwa tuhuma za wizi wa pesa.