Gavana wa Tharaka Nithi Onesmus Muthomi Njuki pamoja na washukiwa wenzake 20 wamefikishwa mahakamani na kukanusha mashtaka ya kuhusika kwenye sakata ya shilingi million 34.9.
Gavana Muthomi pamoja na washukiwa wenzake ambao ni maafisa wa kaunti hiyo pamoja na wafanyibiashara na wamiliki wa kampuni mbalimbali wamekana mashtaka dhidi yao mbele ya hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Douglas Ogoti.
Gavana huyo na wenzake watalala seli usiku wa leo wakisubiri mahakama kutoa uamuzi kuhusu iwapo au la wataachiliwa kwa dhamana Jumatano.