Gavana Korane azuiwa kuingia afisini

0

Gavana Ali Korane na maafisa watano wa kaunti ya Garissa wamefikishwa mahakamani hii leo na kukanusha mashtaka ya ufisadi na utumizi mbaya wa afisi.

Washukiwa hao wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani Douglas Ogot na kukanusha kushirikiana kuiba shilingi Million 233.5.

Kupitia kwa wakili wake Ahmednassir Abdulahi, Gavana Korane ameiambia mahakama kuwa hakuna pesa zozote za kaunti hiyo ambazo zimepotea, kinyume na inavyodaiwa.

Hakimu mkuu wa Mahakama ya Milimani Douglas Ogoti anayeskiliza kesi hiyo amemuachiliwa Gavana Korane kwa shilingi Million 3.25 pesa taslimu huku washukiwa wengine pia wakiachilia kwa shilingi million tano pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 23 mwezi ujao.

Korane azuiwa kuingia afisini

Gavana wa Garissa Ali Korane amekuwa wa hivi karibuni kuzuiwa kuingia afisini baada ya kushtakiwa kwa tuhuma za ufisadi.

Katika uamuzi wake, hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Douglas Ogoti amemtaka Korane kotoingia afisini mwake hadi pale kesi ya ufujaji wa shilingi million 233.5 inayomkabili itakaposkizwa na kuamuliwa.

Korane sasa ni Gavana wa sita kuzuiwa kuingia afisini baada ya magavava Ferdinand Waititu aliyetimuliwa, Mike Sonko wa Nairobi, Moses Lenolkulal wa Samburu, Okoth Obado wa Migori na Muthomi Njuki Tharaka Nithi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here