GACHAGUA AKIMBILIA MAHAKAMANI KUPINGA KUBINIWA KWA BENCHI INAYOSIKILIZA KESI YAKE

0

Naibu Rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua amekata rufaa dhidi ya uamuzi Kuwa Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hakukiuka katiba kwa kubuni jopo la majaji kuskiza na kuamua kesi inayogusana na kutimuliwa kwake afisini.

Gachagua ameitaka Mahakama ya Rufaa kusimamisha kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo imeratibiwa kuanza hapo kesho mwendo wa saa nne asubuhi.

Kupitia mawakili wake Gachagua anadai kuwa ni jaji mkuu pekee yake aliye na jukumu la kubuni jopo la majaji jukumu ambalo haliwezi kutekelezwa na Naibu jaji mkuu (DCJ).

Gachagua ameiambia mahakama ya rufaa kuwa mahakama kuu ilitafsiri katiba visivyo katika uamuzi huo.

“Uamuzi huo ulijikita katika uchanganuzi mbaya wa msingi na mwelekeo wa Katiba,” anasema Gachagua.

Jumatano wiki jana, jopo la majaji watatu likijumuisha Antony Murima , Eric Ogolla na Fridah Mugambi liliamua kuwa Naibu Jaji Mkuu ana uwezo kisheria kubuni jopo spesheli la majaji kwa niaba ya Jaji Mkuu.

Jaji Mrima alisema kuwa Upangaji wa Ratiba ya majaji ni jukumu la usimamizi wa kila siku na unaweza kufanywa na naibu jaji mkuu iwapo Jaji Mkuu hawezi kufanya hivyo.

“Ina uwezekano mkubwa kwamba DCJ anaweza kuwateua majaji chini ya Kifungu cha 165 Kifungu cha 4 cha katiba wakati wowote anapotekeleza majukumu yoyote ya kikatiba kwa niaba ya Jaji Mkuu,” Jaji Mrima alisoma uamuzi huo.

“Katika kesi hii, hatuoni kosa lolote kwa DCJ kuagiza majaji kuketi katika jopo ikizingatiwa kuwa jaji mkuu Mwenyewe haja pinga kubuniwa kwa jopo hili.”

Rufaa hio ni jaribio la hivi karibuni la Gachagua kusaka ridhaa mahakamani akiwa amefeli zaidi ya mara ishirini kusimamisha mchakato wa kutimuliwa afisini na kuapishwa kwa mridhi wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here