Idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona imeongezeka na kufikia 659 baada ya watu 9 zaidi kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi aidha ameripoti kupona kwa watu wengine 198 na hivyo kufikisha idadi hiyo kuwa 24,147.
Idadi ya visa vya ugonjwa huo wa corona vimeongezeka na kufikia 37,218 baada ya watu wengine 139 kupatikana na ugonjwa huo kutokana na sampuli 1,774 zilizopimwa.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifuatwavyo: Nairobi 46, Kisumu 44 Mombasa, Kajiado na Kericho 9, Machakos 3, Nakuru 2, Garisa, Kirinyaka na Kiambu kisa kimoja kila mmoja.
Yakijiri hayo
Familia za watakaopoteza watu wao kutokana na corona sasa zitaruhusiwa kuwazika wapendwa wao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikakati mipya ya kuwazika waliofariki kutokana na ugonjwa huo, katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangani amesema maafisa kutoka wizara afya hawataendelea kuvaa magwanda meupe kama ilivyokuwa awali.
Hata hivyo familia hizo zimetakiwa kuzingatia masharti ya kuzuia msambao wa corona wakati wa mazishi ikiwemo kuvalia barakoa na kutowaruhusu wazee na watoto kuwakaribia marehemu.