Faida ya Safaricom yapungua kwa asilimia 6

0

Faida ya kampuni ya mawasiliano ya Safaricom nusu ya mwaka huu wa kifedha imepungua kwa asilimia sita, ikilinganishwa na kipindi sawia na hicho mwaka uliopita.

Afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa anasema hatua hiyo inatokana na kutotoza ada za kutuma chini ya shilingi elfu moja kwa njia ya Mpesa.

Ndegwa anasema pia kwamba wakenya wengi walipunguza bajeti ya kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kutokana na makali ya janga la corona.

Nusu ya mwaka huu, Safaricom imeandikisha faida ya shilingi billion 33 ikilinganishwa na shilingi billion 35.3 ilizopata kipindi sawia na hicho mwaka uliopita.

Ndegwa ameelezea kuridhika na matokeo hayo ikilinganishwa na makali ya janga la covid19.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here