Mwanauchumi David Ndii pamoja na watu wengine wanne wamewasilisha kesi mahakamani kupinga mchakato wa kurekebisha katiba kupitia BBI.
Ndii ambaye alikuwa mwendani wa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga pamoja na wenzake Jerotich Seii, James Ngondi, Wanjiku Gikonyo na Ikal Angelei wanataka mahakama kutaja kesi yao kama ya dharura.
Kwenye kesi yao, walalamishi kupitia kwa wakili Nelson Havi wanamtaka jaji mkuu David Maraga kubuni jopo la majaji kushughulikia kesi hiyo kwa misingi kwamba inaibua maswala muhimu yenye uzito wa kikatiba.
Walioshtakiwa kwenye kesi hiyo ni mwanasheria mkuu Kihara Kariuki, spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi, mwenzake wa Senate Ken Lusaka pamoja na tuma huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.