Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji ameidhinisha kukamatwa na kushtakiwa kwa aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya bandari nchini KPA Daniel Manduku kwa tuhuma za ufisadi.
Katika taarifa, Haji anasema kuna ushahidi wa kutosha kuwa mamlaka hiyo ilipoteza shilingi million 244 wakati Manduku akihudumu kama mkurugenzi wa mamalaka hiyo.
Haji anasema Manduku pamoja na mshukiwa mwenza Juma Fadhili Chigulu ambaye ni afisa wa mamlaka hiyo walikiuka sheria za ununuzi na kusababisha kupotea kwa pesa za mlipa ushuru.
Washukiwa watafunguliwa mashtaka ya uhalifu wa kiuchumi.