CORONAVIRUS: MAAMBUKIZI ITALIA YAPUNGUA, IDADI YA VIFO YAONGEZEKA

0

Italia kwa siku ya pili mtawalio imeripoti kupungua kwa maafa na maambukizi mapya yanayotokana na virusi vya corona ambayo hadi kufikia sasa yamewaua watu 6, 000 chini ya mwezi mmoja.

Maafa hayo yamepungua kutoka 793 siku ya Jumamosi na kufikia 651 Jumapili na 601 hapo jana Jumatatu.

Idadi ya maambukizi mapya ilipungua kutoka 6, 557 siku ya Jumamosi na kufikia 4, 789.

Idadi kamili ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imefikia 6,077 zaidi ya China na Uhispania ambayo pia yameathirika zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here