CORONAVIRUS: INDIA YAANZA KUTEKELEZA MARUFUKU

0

India imeamkia siku yake ya kwanza ya marufuku ya kutoka nje itakayodumu kwa muda wa majuma matatu yajayo.

Raia wa taifa hilo wamefurika mjini Delhi kununua bidhaa mbalimbali ikiwemo chakula kwa hofu baada ya waziri mkuu Narendra Modi kutangaza hatua kali kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona.

Kwenye hotuba iliyoletwa moja kwa moja kupitia runinga, Modi alisema kwamba ili kuwaokoa raia wa taifa hilo na makali ya virusi hivyo, itakuwa vyema kwa watu kusalia manyumbani mwao la sivyo wataangamia.

India imeripoti visa 519 huku watu 10 wakiripotiwa kupoteza maisha yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here