CORONAVIRUS: HAKUNA MAAMBUKIZI MAPYA CHINA.

0

China haijaandikisha kisa chochote kipya cha virusi vya corona hii leo Ijumaa ndani ya nchi hiyo ikiwa ni siku ya pili kutoandakisha kisa cha ugonjwa huo licha ya kwamba maambukizi mapya 39 yameletwa na raia wanaoingia nchini humo.

Hatua hii inatoa matumaini kwa mataifa mengine duniani yanayoajitihadi kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuweka marufuku ya kutotoka nje.

Aidha, maafa yanayotyokana na corona katika taifa hilo la China yamepungua huku tume ya afya nchini humo ikiripoti vifo vya watu watatu pekee hii ikiwa ni idadi ya chini kwa mara ya kwanza tangu mwezi Januari.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo China ni 3, 248 huku Italia ikiandikisha idadi kubwa ya maafa hadi kufikia sasa ambayo ni 3,400.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here