CORONAVIRUS: AFRIKA KUSINI KUJENGA UKUTA KUDHIBITIA CORONA

0

Afrika Kusini itajenga ukuta kwenye mpaka wake na Zimbabwe kwa muda wa mwezi mmoja ujao ili kuzuia watu walioambukizwa virusi vya corona na wahamiaji wasiokuwa na vibali kuingia nchini humo amesema waziri wa ujenzi Patrcia de Lille.

Ujenzi wa ukuta huo ni miongoni mwa mikakati ya dharura inayowekwa na serikali ya taifa hilo baada ya rais Cyril Ramaphosa kutangaza ugonjwa wa corona kama janga la kitaifa siku ya Jumapili.

Waziri De Lille amesema rais Ramaphosa aliagizwa jufungwa kw amipaka ya taifa hilo ila hilo halitowezekana iwapo ukuta huo hautajengwa.

Afrika Kusini imeripoti visa 150 vya corona wengi wao wakiwa ni raia wake waliokuwa wamesafiri kwenda Italia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here