Idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa corona imeongezeka na kufikia 777 baada ya watu 11 zaidi kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amedhibitisha kuwa watu 97 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 31,097
Watu wengine 73 wamepatikana na virusi hivyo baada ya kupima sampuli 2,001 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 41,619
Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 34, Kilifi 18, Mombasa 11, Busia 4, Taita Taveta 2, Kirinyaga, Kiambu, Meru na Uasin Gishu 1.